• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wapendekeza kufanyika kwa mkutano wa upatanishi wa Libya

    (GMT+08:00) 2019-04-02 09:13:31

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat amependekeza kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa upatanishi wa Libya ili kusuluhisha msukosuko wa kisiasa nchini humo.

    Bw. Mahamat amesema hayo kwenye mkutano na waziri mkuu wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Bw. Fayez Serraj huko Tripoli, ambapo wamejadili maendeleo ya hivi karibuni ya hali ya siasa na usalama nchini humo, pamoja na uchaguzi ujao wa rais na wabunge.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya habari ya Bw. Serraj, inasema mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesisitiza uamuzi kuhusu suala la Libya ni lazima uwe wa Libya, na amekataa hatua za uingiliaji kutoka nje zitakazoufanya msukosuko wa Libya uwe na utatanishi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako