• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ulaya haipaswi kuwa na "hofu ya China"

    (GMT+08:00) 2019-04-02 16:48:33

    Hivi karibuni, Italia na China ilisaini waraka wa kumbukumbu kuhusu ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Jambo hili limewafanya baadhi ya watu wa Ulaya wawe na wasiwasi kuwa, ushirikiano kati ya Italia na China utafarakanisha Umoja wa Ulaya, na nguvu ya ushawishi ya China barani Ulaya itaongezeka kwa haraka. Hii inaonesha kuwa wamekuwa na "hofu ya China".

    China na nchi za Ulaya zinajaribu kujenga dunia yenye ncha nyingi. Kutokana na hali ya utatanishi duniani, pande hizo mbili zinaweza kushirikiana vizuri katika mambo mengi muhimu ya kimataifa. Kwa mfano, baada ya Marekani kujitoa kwenye Makubaliano ya Paris kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa, China na Umoja wa Ulaya zimebeba majukumu ya uongozi, ili juhudi za kukabiliana na suala hilo ziendelee duniani. Na baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano kuhusu suala la nyuklia la Iran, China, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Russia zimeendelea kufuata makubaliano hayo. Katika suala la kulinda utaratibu wa kibiashara wa pande nyingi, China na Umoja wa Ulaya pia zina maoni yanayofanana. Kwa hiyo ushirikiano kati ya China na Ulaya unafanya kazi muhimu isiyokoseka katika kulinda utaratibu wa kimataifa.

    Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara nchini Ufaransa wiki iliyopita alisema, Ulaya yenye mshikamano na ustawi inalingana na matumaini ya China kwa dunia yenye ncha nyingi. Kama Ulaya haina nguvu na mshikamano, nchi nyingine zitakabiliwa na shinikizo zaidi kutokana na vitendo vya upande mmoja. Hivyo maoni kwamba China inataka kufarakanisha Umoja wa Ulaya hayana msingi wowote, na hayalingani na hali halisi.

    Watu wengi wa Ulaya wana wasiwasi kuhusu maendeleo ya kasi ya China. Lakini ukweli ni kwamba, wastani wa mapato ya kitaifa kwa mtu wa China ni Euro elfu saba tu, huku wastani huo wa Umoja wa Ulaya umezidi Euro elfu 35. Bado kuna pengo kubwa la kimaendeleo kati ya China na Ulaya. Maendeleo ya China bila shaka yatapunguza pengo hilo. Lakini ni kweli kuwa Ulaya inastahili kuwa na hofu kuhusu ustawi wa China? Mwenyekiti wa Shirikisho la Mauzo ya Jumla, Biashara na Nje na Huduma la Ujerumani Bw. Holger Bingmann amesema, mashirika ya Ujerumani yanafanya vizuri biashara nchini China, na nchi hiyo imenufaika sana na maendeleo ya uchumi wa China.

    Mwandishi wa habari wa Gazeti la Figaro Bw. Renaud Girard amesema, Umoja wa Ulaya haupaswi kuiogopa China, na adui wa kweli ni ufarakanishaji wa ndani, kupungua kwa kiwango cha elimu na sayansi, na kudidimia kwa sekta ya viwanda.

    Shirikisho la Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la Ujerumani lilizinduliwa tarehe 29 mwezi uliopita. Shirikisho hilo linaona kuwa, Ujerumani itanufaika ikijiunga na pendekezo hilo kwa hatua madhubuti. Mwenyekiti wa Shirikisho la Makampuni ya Ukoo wa Bremen Bw. Peter Bollhagen, kwenye uzinduzi huo alisema makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati ya Ujerumani yanapaswa kuwa na ujasiri wa kushiriki kwenye miradi ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na hii ni fursa kubwa kwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako