• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar : Kamisheni ya utalii Zanzibar yatakiwa kutoka elimu

    (GMT+08:00) 2019-04-02 19:40:05

    Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ameitaka Kamisheni ya Utalii Zanzibar kutoa elimu ya historia ya utalii ili kuujua unakotoka na unakokwenda na hatua zilizofikiwa katika kuimarisha uchumi wa nchi.

    Alisema kuwa kuijua historia ya utalii Zanzibar kutasaidia kwa kiasi kikubwa kujua na kufahamu lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuelewa jinsi utalii ulivyokuwa hapo siku za nyuma na jinsi uliyo hivi sasa na hatua na mafanikio yaliofikiwa kutokana na sekta hiyo.

    Dk. Shein alisema kuwa sekta ya utalii imekuja baada ya zao la karafuu kushuka thamani yake na ndipo marehemu mzee Aboud Jumbe Mwinyi akaona haja ya kuiimarisha sekta hiyo pamoja na baadhi ya mazao mengine ya viungo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako