• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpunga wa GSR wa China unahimiza maendeleo ya kilimo endelevu barani Asia na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-03 08:53:42

    Wanasayansi wa kilimo wa China wamezalisha mbegu kadhaa za mpunga zinazojulikana "Green Super Rice" kwa ajili ya nchi zinazoendelea za Asia na Afrika ili kupunguza njaa na kuongeza mapato ya wakulima.

    Mradi huo unaoungwa mkono na serikali ya China na mfuko wa Bill na Melinda Gates, umezalisha aina 78 za mbegu kwa ajili ya nchi 18 zenye eneo la uzalishaji la hekta milioni 6.12 tangu uanzishwe mwaka 2018, ukiwa na matarajio ya kuwanufaisha wakulima wadogo wa mpunga milioni 30 wa nchi za Asia na Afrika.

    Mkuu wa taasisi ya sayansi za kilimo ya China Bw. Li Zhikang amesema mradi huo unazilenga nchi tisa za Asia, na nyingine tisa za Afrika ambazo ni Msumbiji, Tanzania, Rwanda, Liberia, Ethiopia, Uganda, Nigeria, Mali na Senegal. Timu ya utafiti ya taasisi hiyo imeweza kuongeza uwezo wa mbegu kuvumilia mazingira magumu na kuongeza uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako