• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua uandikishaji wa biometriki wa raia

    (GMT+08:00) 2019-04-03 09:06:59

    Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuzindua uandikishaji wa biometriki wa raia nchini humo, ili kuboresha mipango ya serikali, utoaji wa huduma na usalama.

    Rais Kenyatta amesema Mfumo wa Usimamizi wa Utambulisho wa Taifa (NIIMS) unaoitwa "Huduma Namba" utatoa chanzo pekee cha taarifa binafsi kwa wakenya wote na wageni walioandikishwa.

    Mfumo mpya huo utaunganisha nyaraka zote zilizowekwa na serikali, ambazo ni pamoja na kadi za utambulisho (ID), Mfuko wa Bima ya afya ya Taifa (NHIF), Mfuko wa Usalama wa Jamii wa Taifa (NSSF), vyeti vya kuzaliwa na kifo na Nambari ya Utambulisho binafsi (PIN)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako