• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania aamuru kutoa malipo kwa wakulima wa korosho

    (GMT+08:00) 2019-04-03 09:25:14

    Rais John Magufuli wa Tanzania ameiamuru wizara ya fedha na mpango kutoa shilingi bilioni 50 za Tanzania (sawa na dola milioni 2.6 za kimarekani) kuwalipa wakulima elfu 18 wa korosho katika kanda ya Mtwara, ambao nyaraka zao zimethibitishwa lakini bado hawajapata malipo.

    Rais Magufuli amesema hayo kupitia Shirika la Utangazaji la Tanzania TBC, huku akisema malipo hayo yatatolewa kwa wakulima ambao nyaraka zao zimeshathibitishwa.

    Agizo hilo la rais limetolewa wakati baadhi ya wakulima katika kanda hiyo waliouza bidhaa zao kwa serikali wamelalamikia kuwa hawajalipwa.

    Awali serikali iliahidi kutoa malipo yaliyobaki kwa wakulima hao hadi Machi 31, lakini ilishindwa kufanya hivyo kutokana na kuendelea kwa mchakato wa uhakiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako