• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Robo fainali Klabu Bingwa Afrika: Simba SC wataja viingilio, TP Mazembe kutua jijini Dar leo.

  (GMT+08:00) 2019-04-03 10:04:47

  Klabu ya Simba ya Tanzania imetangaza viingilio katika mchezo wao wa robo fainali klabu bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jumamosi hii April 6.

  Afisa habari wa Wekundu wa Msimbazi Haji Manara amesema kiingilio cha chini kitakuwa ni shilingi 4,000 kwa mzunguko, viingilio vingine ni shilingi 10,000 kwa VIP A, 20,000 kwa VIP B na 100,000 kwa tiketi za Platinum.

  Wakati huo huo, Timu pinzani kwa mchezo huo wazee wa bolingo TP Mazembe ya DRC inatarajiwa kuwasili jijini Dar leo Jumatano tayari kuikabili Simba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako