• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China kutembelea Ulaya

  (GMT+08:00) 2019-04-03 16:55:20

  Kuanzia tarehe 8 hadi 12, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atahudhuria mkutano 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya mjini Brussels, na mazungumzo ya 8 ya viongozi wa China na nchi za Ulaya ya mashariki na kati nchini Croatia, na kufanya ziara rasmi nchini Croatia. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Chao amesema, ziara hii itafanywa baada ya ziara ya rais Xi Jinping wa China barani Ulaya, na kuonesha kuwa China inatilia maanani sana uhusiano wake na Ulaya.

  Baada ya ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Italia, Monaco na Ufarasa, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atafanya ziara barani Ulaya wiki ijayo. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Chao anasema,

  "Rais Xi na waziri mkuu Bw. Li Keqiang wote wamechagua Ulaya kufanya ziara yao ya kwanza mwaka huu, hali hii inaonesha kuwa China inatilia maanani uhusiano wake na Ulaya. "

  Mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya utafanyika tarehe 9 mjini Brussels, na Bw. Li, mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Junker watabadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa yanayofuatiliwa na pande hizo mbili, na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano.

  Mazungumzo ya 8 ya viongozi wa China na nchi za Ulaya ya mashariki na kati yenye kauli mbiu ya "kujenga daraja la kufungua mlango, uvumbuzi na wenzi" yatafanyika tarehe 12 Dubrovnik nchini Croatia. Bw. Wang anasema,

  "Mazungumzo hayo yatatoa nyaraka za matokeo, na kutunga mpango wa ushirikiano wa "16+1". Aidha pande hizo mbili pia zitasaini makubaliano kuhusu ushirikiano wa ujenzi wa miundo mbinu, biashara, fedha, elimu, ukaguzi wa sifa za bidhaa, urahisishaji wa kutembeleana kwa watu na kutambuliana lesensi ya dereva."

  Kuhusu ziara rasmi ya Bw. Li nchini Croatia, Bw. Wang amesema, nchi hiyo ilikuwa kituo muhimu cha njia ya hariri ya kale, na sasa ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya na nchi muhimu ya Ulaya ya mashariki na kati. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa China kufanya ziara nchini Croatia tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi. Bw. Wang anasema,

  "Katika ziara hiyo, Bw. Li atafanya mazungumzo na rais, waziri mkuu na spika wa bunge la Croatia, na kubadilishana nao maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ushirikiano wa '16+1', kujenga kwa pamoja 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', uhusiano kati ya China na Ulaya, na masuala mengine yanayofuatiliwa na pande hizo mbili."

  Bw. Wang amesema, hivi sasa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya yana mwelekeo mzuri, na pande hizo mbili zina maslahi mengi ya pamoja katika kukuza ushirikiano wa kunufaishana, msimamo wa pamoja katika kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, lengo la pamoja katika kukamilisha usimamizi wa dunia na kulinda amani na utulivu duniani. Anaamini kuwa ziara ya Bw. Li itainua zaidi kiwango cha uhusiano kati ya China na Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako