Roketi ya kwanza ya kubeba mizigo kwa matumizi ya kibiashara imemaliza majaribio ya injini, na kutoa njia kwa ajili ya safari yake ya kwanza katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa Chuo cha Teknolojia ya Kutengeneza Magari cha China (CALT), roketi hiyo iitwayo Smart Dragon-1 ni kizazi cha kwanza cha mfululizo wa roketi za kubeba mizigo zitakazotengenezwa na CALT.
Chuo hicho kimesema, imechukua miezi sita kutengeneza roketi hiyo na saa 24 kuiandaa kwa kurushwa, na inaweza kutumika kwa kurusha setilaiti moja ama setilaiti kadhaa kwa wakati mmoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |