• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 268 wamefariki nchini Zimbabwe kutokana na kimbunga Idai

  (GMT+08:00) 2019-04-03 18:55:46

  Waziri wa huduma za habari, uenezi na raido wa Zimbabwe Bibi Monica Mutsvangwa amesema, watu 268 wamefariki na mamia ya wengine hawajulikani walipo kufuatia kimbunga Idai kilichoshambulia sehemu ya mashariki ya Zimbabwe katikati ya mwezi uliopita.

  Bibi Mutsvangwa aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maafa yaliyosababishwa na kimbunga Idai. Amesema kazi za uokoaji zinaendelea na inakadiriwa kuwa miili zaidi ya watu waliofariki itagunduliwa.

  Amesema idara husika inakarabati njia ya kwenda eneo lililokumbwa na maafa ili kuhakikisha vifaa vya uokoaji vinawafikia watu walioathiriwa na kimbunga hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako