• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka pande mbalimbali kulinda amani na usalama wa anga ya juu

    (GMT+08:00) 2019-04-03 19:10:58

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China inasikitishwa na kutopitishwa kwa ripoti ya waraka wa sheria ya kimataifa ya kuzuia mashindano ya vifaa vya kijeshi kwenye anga ya juu.

    Bw. Geng Shuang amesema, China inataka pande mbalimbali zishiriki kwenye mchakato wa udhibiti wa mambo ya kijeshi na kulinda amani na usalama wa kudumu wa anga ya juu. Ameongeza kuwa, kuzuia mashindano ya vifaa vya kijeshi kwenye eneo hilo ni matakwa ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, na China siku zote inatetea kutumia anga ya juu kwa amani, na kupinga mashindano ya vifaa vya kijeshi na kuvifanya kuwa silaha kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako