• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa kwanza ajiuzulu nchini Uingereza baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo kutafuta mazungumzo na kiongozi wa upinzani kuhusu Brexit

    (GMT+08:00) 2019-04-03 19:28:58

    Waziri wa Uingereza anayeshughulika na Wales Bw. Nigel Adams amejiuzulu wadhifa wake baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Theresa May kutangaza mpango wake wa kuongea na kiongozi wa chama cha upinzani cha Labor Bw. Jeremy Corbyn ili kumaliza mvutano kuhusu suala la Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Bw. Adams amekuwa ofisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa serikali kujiuzulu kufuatia mfululizo wa mkutano wa baraza la mawaziri. Katika barua yake, Bw. Adams amemtuhumu waziri mkuu kwa kutafuta makubaliano na Bw. Corbyn ambaye hajawahi katika historia yake ya kisiasa kutanguliza maslahi ya Uingereza.

    Waziri mkuu Theresa May anatarajiwa kukutana na Bw. Corbyn kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako