• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 13 wa naibu mawaziri wa mazungumzo ya uhusiano wa wenzi wa kiuchumi kati ya China na Japan wafanyika

  (GMT+08:00) 2019-04-03 19:37:08

  Mkutano wa 13 wa ngazi ya naibu mawaziri wa mazungumzo ya uhusiano wa wenzi wa kiuchumi kati ya China na Japan umefanyika leo hapa Beijing na kuendeshwa kwa pamoja na naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming na naibu waziri wa mambo ya nje wa Japan Yamazaki Kazuyuki.

  Pande hizo mbili zimebadilishana maoni kuhusu hali ya jumla ya uchumi wa dunia na nchi hizo mbili, mazungumzo ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika biashara, uwekezaji, soko la upande wa tatu, na uvumbuzi. Pia wamejadiliana kuhusu mambo ya fedha, uhifadhi wa mazingira, huduma kwa wazee, utalii na sekta nyingine, mkataba wa uhusiano wa kiwenzi na kiuchumi wa kikanda kwa pande zote, pamoja na eneo la biashara huria la China, Japan na Korea Kaskazini, mageuzi ya WTO, mkutano wa kundi la nchi 20 na masuala mengine ya ushirikiano wa kikanda na wa pande nyingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako