• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU na NATO kuimarisha ushirikiano katika kuendesha Vikosi vya Akiba vya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-04 09:09:58

    Umoja wa Afrika na Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO wametoa wito wa kuongeza ushirikiano katika kuendesha Vikosi vya Akiba vya Afrika ASF.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema maofisa wa pande hizo mbili wametoa wito huo kufuatia mkutano wa Kamishna wa Umoja huo anayeshughulikia Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia Bibi Sarah Anyang Agbor na kamanda wa majeshi washirika ya mseto na kamanda wa jeshi la majini la Marekani barani Ulaya na Afrika Bw. James G. Foggo III. Mkutano huo uliofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa umetambua umuhimu za kukuza ushirikiano kati ya pande hizo katika masuala yanayohusu mawasiliano ya kisiasa, ujenzi wa uwezo na ushirikiano kati ya mabara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako