• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kanda ya Afrika Mashariki yaahidi kuchukua hatua kuhusu matishio ya usalama yanayokabili ghuba ya Aden

    (GMT+08:00) 2019-04-04 09:38:21

    Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD itachangia rasilimali za watu na fedha kwa miradi inayolenga kuimarisha usalama katika bahari ya Sham na ghuba ya Aden.

    Katibu mkuu wa jumuiya ya IGAD Bw. Mahboub Maalim amesema, kulinda bahari ya Sham na ghuba ya Aden kutokana na matishio ya asili na yanayoletwa na binadamu, ni muhimu katika kuzidisha ukuaji wa kiuchumi, usalama na amani katika kanda ya Pembe ya Afrika.

    Amesema hayo katika mkutano wa kwanza wa kikosi kazi cha jumuiya hiyo kuhusu bahari ya Sham na ghuba ya Aden kilichotolewa na mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya hiyo katika mkutano wa kilele uliofanyika mwezi Februari, ili kutoa uzoefu unaohitajika kutatua matishio yanayokabili njia muhimu ya meli.

    Pia amesema wamefikia makubaliano kuhusu haja ya kutatua changamoto za usalama zinazoikabili ghuba ya Aden, ambayo ni njia muhimu ya baharini. Kipaumbele chao ni kupambana na ugaidi, uvuvi haramu na utupaji wa taka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako