• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yasema watalii wa China walichangia dola za kimarekani milioni 190 kwa pato lake 2018

    (GMT+08:00) 2019-04-04 09:42:32

    Serikali ya Ethiopia imesema imepata pato la dola za kimarekani milioni 190 kutoka kwa watalii wa China waliotembelea nchi hiyo mwaka 2018.

    China ni chanzo kikuu cha tatu cha watalii wanaotembelea Ethiopia, ikizifuata Marekani na Uingereza. Idadi ya watalii waliotembelea Ethiopia mwaka 2018 imefikia 45,307, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.7 kuliko ile ya mwaka 2017.

    Mkurugenzi wa Idara ya Umma na Mahusiano ya Kimataifa kwenye Wizara ya Utamaduni na Utalii Bw. Gezahegn Abate amesema chakula kizuri na vifaa vizuri vya malazi vitawavutia zaidi watalii wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako