• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbegu za mpunga aina ya GSR yanufaisha wakulima wa Asia na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-04 16:51:03

    China iko mbele duniani kwa teknolojia ya mbegu za mpunga. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, mbegu za mpunga aina ya Green Super Rice GSR zilizotengenezwa na wanasayansi wa China zimenufaisha zaidi ya familia milioni 1.6 za wakulima wa nchi za Asia na Afrika.

    Mradi wa kutoa mbegu za mpunga wa GSR kwa sehemu maskini za Asia na Afrika ulioendeshwa na wanasayansi wa China umemalizika mwanzoni mwa mwezi huu. Mradi huo wa kimataifa wa kupunguza umaskini kupitia teknolojia za kilimo ulianzishwa mwaka 2008, na katika miaka 11 iliyopita, wanasayansi wa China wamefanikiwa kutengeneza aina nyingi za mbegu za mpunga ambao unaweza kuongeza mazao na kupunguza uchafuzi kwa mazingira. Mwanasayansi mkuu wa mradi huo Bw. Li Zhikang ambaye pia ni mtafiti wa taasisi ya utafiti wa mimea ya kilimo ya Akademia ya Teknolojia za Kilimo ya China anasema,

    "Tulitathmini na kueneza aina 78 za mbegu za mpunga, na mbegu hizo zilizopandwa katika zaidi ya mashamba hekta milioni sita zimenufaisha zaidi ya familia milioni 1.6 za wakulima."

    GSR ni mbegu bora ya mpunga ambayo inayoweza kupunguza matumizi ya dawa, mbolea na maji, huku ikitoa mavuno mazuri. Mazao endelevu ya mpunga ni muhimu zaidi kwa nchi nyingi za Asia na Afrika katika kuhakikisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini. Mtafiti wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mpunga ya Philippines Dr. Jauhar Ali amesema, kueneza mbegu za GSR kumesaidia wakulima wa nchi hiyo kuongeza mazao na kupunguza umaskini. Anasema,

    "Wakulima wa Philippines wanaridhika sana na mavuno ya GSR. Hivi sasa tumepanda GSR katika hekta milioni moja za mashamba, na wastani wa ongezeko la kipato cha wakulima kwa hekta moja ni dola 200 za kimarekani. Hii ni faida kubwa kwa jamii yetu."

    Hivi sasa mradi wa kutoa mbegu za mpunga aina ya GSR kwa sehemu maskini za Asia na Afrika umemalizika, lakini baadhi ya nchi za Afrika zilizonufaika na mradi huo zinapenda kuendelea na ushirikiano na China. Mtafiti wa taasisi ya kitaifa ya nafaka ya Nigeria Dr. Ishaq Mohammed anasema,

    "Hadi sasa karibu makampuni 20 ya mbegu ya nchi yetu yametumia mbeza GSR. Tunajitahidi kupanua mashamba ya kupanda mbegu za GSR, ili kuongeza mazao ya mpunga."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako