• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya ngazi ya juu ya NATO yaanza licha ya mvutano

  (GMT+08:00) 2019-04-04 18:38:18

  Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) wamekutana mjini Washington, Marekani jana kwa mkutano wa siku mbili katika kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ya kijeshi, huku Russia ikiwa ajenda kuu ya mkutano huo.

  Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Bw. Jens Stoltenberg amesema, majadiliano kati ya viongozi hao yatalenga kutafuta mkakati wa kukabiliana na tishio la Russia. Amesema hivi sasa dunia haitaki kuwa na mbio mpya za silaha, na wala hakuna haja ya kuwa na Vita mpya ya Baridi, na kuongeza kuwa NATO haina nia ya kuitenga Russia, bali inatafuta uhusiano mzuri na nchi hiyo.

  Bw. Stoltenberg pia ametoa wito wa mshikamano wa jumuiya hiyo huku akikiri kuwepo kwa tofauti kubwa ambayo inaweza kuonekana katika mikutano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako