• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapitisha miswada kadhaa ya marekebisho ya sheria kwa ajili ya utekelezaji wa sheria ya uwekezaji kutoka nje

  (GMT+08:00) 2019-04-04 19:07:37

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana ameendesha mkutano wa baraza la serikali ya China, ambao umepitisha miswada kadhaa ya marekebisho ya sheria kwa ajili ya utekelezaji wa sheria ya uwekezaji kutoka nje na kuendana na mahitaji ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara.

  Mkutano huo umeamua kupunguza kodi ya mizigo na vitu binafsi, ili kuhimiza kupanua uagizaji bidhaa na matumizi kutoka nje. Kuanzia tarehe 9 mwezi huu, kiasi cha kodi ya mizigo na vitu zinazoingia China kwa mtu binafsi kitapunguzwa, kodi ya bidhaa za chakula na dawa itapungua hadi asilimia 13 kutoka asilimia 15, na kodi za bidhaa za nguo na vifaa vya umeme zitapungua hadi asilimia 20 kutoka asilimia 25.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako