• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa kanda ya Afrika Mashariki kukua kwa asilimia 5.9 mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-04-04 19:11:11

    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema kupungua kwa pato linalotokana na usafirishaji wa bidhaa zikiwemo madini kumesababisha kushuka kidogo kwa ukuaji wa uchumi katika eneo la Afrika Mashariki kwa mwaka jana.

    Ripoti iliyotolewa na benki hiyo jana imesema, ukuaji wa uchumi katika eneo hilo unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka huu na asilimia 6.1 kwa mwaka ujao. Benki hiyo inakadiria ukuaji huo wa uchumi utatokana na matumizi ya ndani ya bidhaa na ukuaji katika sekta ya huduma.

    Hata hivyo, Benki hiyo imeeleza wasiwasi wake kutokana na kukua kwa kiwango cha kuongezeka kwa madeni kwa nchi ambazo awali zilifaidika kwa kusamehewa madeni yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako