• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonyesho ya pili ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje kualika zaidi kampuni binafsi na kampuni ndogo na za ukubwa wa kati

  (GMT+08:00) 2019-04-04 19:21:31

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo amesema, China itaalika zaidi kampuni binafsi na zenye ukubwa wa kati na ya ndogo na kujitahidi kuwaalika wafanyabiashara kutoka nje kushiriki kwenye maonyesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje.

  Bw. Gao Feng amesema mpaka sasa kampuni zaidi ya 1,800 zimejisajili kushiriki kwenye maonyesho hayo na kuongeza kuwa, maandalizi ya maonyesho hayo yanafanyika kwa taratibu.

  Wizara ya biashara ya China itaendelea kuhimiza kazi husika, na kuandaa vizuri baraza la uchumi wa kimataifa la Hongqiao, ili kuhakikisha maonyesho hayo yanafanyika kwa mafanikio.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako