• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali kuunganisha huduma ya bure ya intanenti katika bustani ya Mama Ngina

    (GMT+08:00) 2019-04-04 19:49:57

    Serikali kuu nchini Kenya inapanga kuunganisha huduma ya bure ya intaneti kwa watakaokuwa wakizuru bustani ya kisasa ya Mama Ngina ambayo ujenzi wake unaendelea mjini Mombasa.

    Katibu Mkuu katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia,Jerome Ochieng amesema hatua hii itawapatia watalii fursa ya kufurahia mandhari ya bustani hiyo huku wakipiga picha na video na kuzisambaza kwa kutumia intaneti ya bure itakayopatikana katika bustani ya Mama Ngina.

    Aidha Jerome alisema sio tu watalii watakaofaidika bali pia wafanyabiashara katika eneo hilo.

    Mradi huu unaogharimu takriban milioni Sh460 ulizinduliwa Januari mwaka huu na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wengine.

    Ujenzi wa bustani hiyo unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako