• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar:Serikali imeweka mikakati ya kuwainua wajasiriamali

    (GMT+08:00) 2019-04-04 19:51:42

    Serikali ya Zanzibar imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawanyanyua kiuchumi wajasiriamali ili kuweza kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.

    Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Ajira Zanzibar, Ali Suleiman Ameir.

    Amir aliyasema hayo jana katika kiwanja cha kumbukumbu Kisonge wakati alipokuwa akifunga maonyesho ya kwanza ya kazi za wajasiriamali yalioandaliwa na Mtandao wa Tamaduni za Kijamii Zanzibar.

    Alisema kuanzishwa kwa mfuko wa uwezeshaji, idara ya programu za uwezeshaji na vituo vya kuwaendeleza wajasriamali kumesaidia baadhi ya wananchi hususan vijana kupata mbinu mbadala za kujiajiri.

    Aidha, aliwataka wajasiriamali hao kutovunjika moyo kutokana na matatizo madogo yanayojitokeza na badala yake wazidishe juhudi ili kuweza kufikia malengo waliojipangia ya kujikomboa na umaskini.

    Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kuthamini bidhaa za wajasiriamali wa ndani badala ya bidhaa kutoka nje ya nchi wakati bidhaa hizo zinapatikana nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako