• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNDP na IGAD wazindua ofisi ya forodha ili kuimarisha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2019-04-05 08:27:06

    Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na Shirika la maendeleo ya kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD wamefungua ofisi kwenye mpaka kati ya Kenya na Ethiopia, ili kuhimiza utatuzi wa migogoro, amani na maendeleo kati ya nchi hizo mbili.

    Ofisa wa kikanda wa UNDP Bw Matteo Frontini, amesema ofisi hiyo pia itahimiza biashara na kuishi kwa masikilizano kati ya jamii za watu wanaoishi kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.

    Kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi Bw. Frontini amesema ofisi hiyo pia itasaidia kutatua mambo yanayochochea migogoro na kutokuwepo kwa utulivu, uhamiaji usio wa kawaida na watu kutokuwa na makazi katika maeneo ya mpakani.

    Ofisi hiyo inatarajiwa kuhudumia maeneo ya kusini magharibi mwa Ethiopia, Kaskazini magharibi mwa Kenya na Somalia, ili kuhakikisha jamii zinaopakana zinashiriki kwenye shughuli za maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako