• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wapongeza juhudi za China kwenye sekta ya Afya

    (GMT+08:00) 2019-04-05 08:27:47

    Kituo cha kupambana na maradhi cha Umoja wa Afrika CDC kimepongeza juhudi za China kwenye kusaidia sekta ya afya barani Afrika, hasa kwenye kupambana na ugonjwa wa malaria.

    Mkuu wa sera na diplomasia ya afya wa CDC Bw Benjamin Djoudalbaye, amesema China imekuwa inafanya kazi nyingi katika kusaidia kupambana na magonjwa hatari kama vile Malaria.

    Ameitaja dawa ya kupambana na Malaria aina ya Artemisinin iliyogunduliwa na China, kuwa ni dawa yenye ufanisi mkubwa kwenye kupambana na ugonjwa huo.

    China imekuwa ikilisaidia bara la Afrika kwenye sekta ya afya kupitia mpango wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na ikiwa ni sehemu ya msaada wake, China inatuma vikundi vya madaktari katika nchi mbalimbali za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako