• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Derby ya Der Klassiker kupigwa Jumamosi hii dimba la Allianz Arena.

  (GMT+08:00) 2019-04-05 09:32:01

  Katika ulimwengu wa soka kuna mechi chache sana zinazoweza kuamsha hisia kama derby ya Der Klassiker ambayo itapigwa Jumamosi hii katika dimba la Allianz Arena nyumbani kwa Bayern Munich. Ni bonge moja la mechi ambayo ni zaidi ya derby ya kawaida kwa sababu timu zote mbili zinawania ubingwa wa Bundesliga.

  Borussia Dortmund walirejea kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa dakika za lala salama kwa mabao 2-0 dhidi ya Wolfsburg, huku Bayern wakidondosha alama mbili baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini kwa Freiburg, mchezo huo utaifanya Bayern Munich kupanda kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo endapo tu watashinda. Borussia Dortmund wao wanatakiwa kuepuka kufungwa ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa Bundesliga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako