• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Michuano ya kufuzu Olimpiki 2020 Japan- Twiga Stars kamili gado kuikabili Leopards ya DRC

    (GMT+08:00) 2019-04-05 09:33:23

    Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) Bakari Shime amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa taifa jijini Dra es Salaam leo Ijumaa kuwashangilia Twiga Stars watakapoikaribisha the Leopards ya DRC katika kuwania kufuzu fainali za Olimpiki zitakazofanyika Japan mwaka 2020.

    Shime amesema wachezaji wa Twiga Stars wako tayari kwa mchezo huo isipokuwa Asha Hamza aliyeumia akiwa mazoezini. Naye kocha wa Leopards Kadiamba Marcello amesema wamekwenda Tanzania kupambana na kushinda, lakini kikubwa watazuia kuona hawaruhusu goli lolote nyavuni mwao.

    Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wananchi kkwenda kwa wingi uwanjani kuzipa nguvu Twiga Stars pamoja na Simba Sports Klabu ambazo zinapeperusha bendera ya taifa hilo kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako