• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wakumbuka watu waliofariki katika siku ya Qingming kwa njia mwafaka

    (GMT+08:00) 2019-04-05 17:12:11

    Leo tarehe 5, Mei ni siku ya Qingming ya China, ambayo ni siku ya wachina kuwakumbuka mababu, wanafamilia au marafiki zao waliofariki dunia. Katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi wanachagua njia mwafaka kuadhimisha siku hii ili kupunguza athari kwa mazingira.

    Wachina wana desturi ya kuchoma mali za bandia zilizotengenezwa kwa karatasi ili kuwakumbuka watu waliofariki dunia, ambao wanaaminiwa kuishi katika dunia nyingine na kuhitaji mali hizo. Katika miaka ya hivi karibuni, badala ya kufanya hivyo, wachina wengi wanatoa maua kwa ndugu zao waliofariki dunia katika siku ya Qingming, ili kupunguza uchafuzi kwa mazingira na ajali ya moto.

    Serikali ya wilaya ya Longhua mkoani Hebei imeanzisha vituo 18 vya kutoa maua ya bure katika siku ya Qingming. Bw. Wang Yulong kutoka kijiji cha Gangwayaogou cha wilaya hiyo alifika kwenye kituo hicho mapema ili kuchukua maua. Anasema,

    "Wakati wa sikukuu ya Qingming, watu wote wanaenda kwenye makaburi ya mababu zao ili kuwakumbuka. Zamani tulichoma pesa bandia za karatasi, na sasa tunatumia maua. Kwani maua hayasababishi uchafuzi na ajali za moto. Ni afadhali tubadilishe mawazo yetu."

    Aidha, baadhi ya vijana wa China wameanza kukumbuka watu waliofariki kupitia tovuti za mtandao katika siku ya Qingming. Hii ni njia rahisi kwa watu wanaofanya kazi nje ya nyumbani kwao.

    Wakati huo huo, njia ya mazishi pia imebadilika nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na upungufu wa makaburi, njia nyingine za mazishi kwa vile mazishi ya mti, mazishi ya tuta la maua au nyasi, na mazishi ya mtoni yanaenezwa katika sehemu mbalimbali. Meneja wa Eneo la Makaburi la Gongde la mji wa Nanjing Bw. Ye Zhengsheng, amesema eneo hilo lina sehemu maalumu ya mazishi, ambayo watu waliofariki na kuzikwa hapa kwa njia ya isiyo na uchfuzi. Hadi sasa sehemu hiyo yenye mita 200 za mraba imezikwa watu zaidi ya 9,000. Bw. Ye anasema,

    "Majivu ya watu waliofariki yakizikwa chini ya mti, yatatoweka baada ya miezi mitatu. Pia tuna mazishi ya tuta la maua na nyasi. Mwaka jana, mazishi kwa njia isiyosababisha uchafuzi kwa mazingira yamechukua zaidi ya asilimia 60 katika eneo letu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako