• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya ujenzi ya Dodoma kufanyika Juni 7 hadi 8

    (GMT+08:00) 2019-04-05 19:06:10

    Maonyesho ya wadau wa sekta ya ujenzi yajulikanayo kama Dodoma Builders Expo kwa ajili ya kuhamasisha viwanda, yamepangwa kufanyika Juni 7 hadi 8 jijini mwaka huu.

    Katika maonyesho hayo, kampuni 100 zinatarajia kushiriki pamoja na watazamaji 12,000 wakitarajia kuhudhuria.

    Akizungumza jana jijini Dodoma Mkurugenzi wa Dodoma Builders Expo, Atatenda Nyawo, alisema hayo ni maonyesho ya pili kufanyika, ambapo yanatarajia kushirikisha wadau mbalimbali.

    Tatenda alisema jumla ya wadau 100 watashiriki maonyesho hayo huku akiwataka watu kujitokeza katika maonyesho hayo.

    Alifafanua kuwa maonyesho hayo yataleta faida kubwa kwa Watanzania kwa sababu vijana wengi watafanikiwa kupata ajira.

    Alisema inafahamika Dodoma ni makao makuu, kwa hiyo wanaungana na serikali kuijenga.

    Naye mratibu wa maonyesho hayo, Albert Makoye, alisema yatawasaidia wadau wa ujenzi kuzitangaza bidhaa zao kwa jamii.

    Alisema mwaka huu kutakuwa na maboresho makubwa na washiriki wengi wanatarajia kushiriki katika maonyesho hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako