• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zinatarajiwa kubeba kwa pamoja wajibu kwa dunia

    (GMT+08:00) 2019-04-06 17:17:31

    Siku ya Alhamisi rais Donald Trump wa Marekani alipokutana na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He, aliyeongoza ujumbe wa China katika mazungumzo ya kibiashara ya duru la 9 kati ya China na Marekani, alisema anapenda kuona pande mbili zinafikia makubaliano ya kihistoria ya pande zote mapema iwezekanavyo, hali ambayo si kama tu itazinufaisha Marekani na China, bali pia dunia nzima. Vile vile alipojibu swali la mwandishi wa habari wa Shirika la vyombo vya habari la China CMG. Rais Trump alisema Marekani na China zina wajibu kwa dunia.

    Tumeona rais Xi Jinping wa China akisisitiza mara kwa mara kuwa, "China na Marekani zina wajibu mzito wa pamoja katika kuhimiza amani na ustawi ulimwenguni." Safari hii katika ujumbe uliokabidhiwa kwa rais Trump, rais Xi alisisitiza kuwa hivi sasa uhusiano kati ya China na Marekani unaoendelea kwa hatua madhubuti, unahusisha maslahi ya watu wa nchi hizi mbili, pamoja na mataifa mengine duniani, ndio maana viongozi wa nchi hizo mbili wanapaswa kuonesha uwezo wa uongozi wa kimkakati. Tunaona kauli ya rais Trump kuhusu wajibu kwa dunia ni jibu kwa ujumbe huo wa rais Xi.

    Kihalisi dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea kwa karne. Kutokana na haliya sasa, mataifa mbalimbali yanatarajia China na Marekani zikiwa ni nchi zenye ushawishi mkubwa, zinaweza kubeba wajibu wa pamoja kwa dunia katika kazi tatu.

    Ya kwanza ni maendeleo. Maendeleo ya kipaumbele ya walimwengu wa hivi leo. Lakini mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani iliyozuka mwaka jana, imepunguza kasi ya ongezeko la uchumi duniani. Hivi karibuni Shirika la biashara duniani WTO lilipunguza makadirio ya ongezeko la uchumi duniani kwa mwaka huu kutoka 3.7% hadi 2.6%. Endapo makubaliano ya kibiashara yatafikiwa kati ya China na Marekani, hakika yatawatia moyo walimwengu na kuchangia kazi ya maendeleo duniani.

    Ya pili ni Amani. Katika nafasi ya wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, China na Marekani zina wajibu wa kuleta uhakika na utulivu zaidi ulimwenguni. China imetangaza kuwa kuanzia tarehe mosi Mei, dawa zote aina ya Fentanyl zitawekwa chini ya usimamizi. Rais Trump aliishukuru China kutokana na hatua hiyo, kwamba ina maana kubwa kwa wananchi wa Marekani na ushirikiano wa kupambana na dawa za kulevya kati ya Marekani na China.

    Ya tatu ni usimamizi wa mambo duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, mfumo wa utaratibu wa mambo duniani ulioanzishwa baada ya kumalizika kwa vita vikuu vya pili duniani, umekuwa unakabiliwa na changamoto kubwa, huku dunia ikishuhudia kuibuka kwa mawazo ya kuchukua hatua kwa kuzingatia maslahi ya upande mmoja tu, kujilinda kibiashara, n.k. Chukua mfano wa mageuzi ya shirika la WTO, nchi mbalimbali zilishauri lifanyiwe mageuzi, huku China na Marekani kila moja ikiwa na mapendekezo yake. Lakini hatua za mageuzi zinapaswa kuamuliwa baada ya mashauriano ya pande mbalimbali, ili kulinda mfumo wa biashara ya pande zote, na kulinda maslahi ya nchi na sehemu zinazoendelea.

    Hivi sasa mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yameingia katika duru la 9. Cha muhimu zaidi ni kudhibiti maoni tofauti na kupanua wigo wa ushirikiano, jambo ambalo si kama tu linalingana na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili, bali pia ni wajibu kwa dunia ambao nchi hizo mbili kubwa zinapaswa kuubeba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako