• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kufungua ubalozi mdogo Guangzhou, China

    (GMT+08:00) 2019-04-07 15:18:21

    Urafiki na ushirikiano wa miaka mingi baina ya China na Tanzania umeendelea kuimarika kila kukicha kwa kuwepo ushirikiano wa masuala ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

    Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kinabaiinisha kuwa China inaendelea kuongoza kwa kuweka mitaji mikubwa nchini Tanzania kwa zaidi ya dola Bilioni 5.8 Duniani katika uwekezaji kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017.

    China ina miradi 723 ikitoa ajira 87,126 kwa thamani ya dola Milioni 5 962.74, ikifuatiwa na Uingereza yenye miradi 936 iliyozaa ajira 274,401 kwa thamani ya dola Milioni 5,540.07 na Marekani ikiwa na miradi 244 iliyozalisha ajira 51,880 kwa thamani ya dola Milioni 4,721.15.

    Hatua hiyo, inafanya pia Tanzania kuwa mshirika mkubwa wa biashara kwa watanzania wengi kufanya biashara katika miji mbalimbali nchini China lakini kwa kiasi kikubwa biashara zikifanyika katika mji wa Guangzhou.

    Katika mji huo wa kibiashara kwa waliofika watakubaliana nami kuwa ni hakika ni Afrika ya China kwa jinsi kulivyo na waafrika wengi wanaofika na kufanya biashara huku wengine wakiweka makazi yao ya kudumu.

    Aidha,kuna baadhi ya maeneo utakutana na watanzania wakiendesha maisha yao huku lugha yao kuu ikiwa ni Kiswahili,hivyo kujiona kama umefika nchini Tanzania na hata unapouliza mgahawa kwa ajili ya Chakula utaelekezwa katika mgahawa maarufu wa Kilimanjaro wenye vyakula vyenye asili ya Afrika hususan Tanzania.

    Ingawa nchini China kuna ubalozi wake huko Beijing lakini serikali kwa kuona umuhimu wa kuwahudumia wananchi wake wanaoshi na kufanya biashara katika maeneo hayo wametangaza kufungua kwa ubalozi mdogo.

    Serikali kupitia Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi imeeleza inatarajia kufungua ubalozi mdogo wa Tanzania katika mji wa Guangzhou nchini China.

    Pia ameeleza kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) katikkati ya mwaka huu inatarajia kuanza safari zake kati ya Dar es Salaam na mji huo wa kibiashara hivyo wasafiri kuhudumiwa na ubalozi huo mdogo.

    Hatua hiyo imefikiwa kwa kuzingatia ushirikiano katika masuala mbalimbali uliopo baina ya China na Tanzania ikiwemo mji huo kuwa na mzunguko mkubwa kwa watanzania wanaofanyabiashara baina ya pande hizo mbili.

    Kabudi, anasema wizara yake katika bajeti yake ya mwaka 2019/2020 wameiomba bunge kulidhia kufungua ubalozi mdogo katika mji huo wa kibiashara nchini humo utakaokuwa na balozi mdogo na kufanya shughuli zote za kibalozi.

    Kufunguliwa kwa ubalozi mdogo utasaidia kurahisisha huduma kwa watanzania pamoja na wawekezaji toka China wanaotokea katika mji huo wa biashara na mingine iliyo karibu.

    Kabudi anasema pia wanatarajia kufungua ubalozi mwingine mdogo katika mji wa Lubumbashi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

    Alisema Tanzania kuwa na ubalozi mdogo ni jambo la kawaida kwani katika nchi za falme zakiarabu na nyinginezo kwa kuzingatia ukubwa wa nchi na wingi wa watanzania wanaofanya huduma mbalimbali katika nchi hiyo.

    Waziri anasema ubalozi huo mdogo utaimarisha shughuli zake zaidi kwa wafanyabiashara pamoja na kutoa huduma za shirika la ndege Tanzania ATCL linalotarajia baadaye mwaka huu kuanza safari za kwenda Guangzhou nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako