• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaadhimisha "Qingming Festival" kwa kuwakumbuka raia wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa TAZARA

    (GMT+08:00) 2019-04-07 15:22:25

    Ijumaa April 5, mwaka huu Tanzania iliungana na China kuadhimisho sikukuu za kijadi ijulikanayo kama "Qingming Festival" pia inatambulika kama siku ya kufagia makaburi na kukumbuka watu mbalimbali waliokufa.

    Katika maadhimisho ya sikukuu hiyo ya kijadi,nchini China wananchi wanakuwa mapumziko kwa siku kadhaa na wengi huenda katika maeneo ya vijiji na walikozaliwa kwa ajili hiyo.

    Jijini Dar es Salaam, Balozi wa China nchini Wang Ke akishirikiana na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof. Palamagamba Kabudi, waliongoza raia wa China nchini na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wakuu kuadhimisha siku hiyo.

    Katika Maadhimisho hayo, yalitumiwa kuwakumbuka raia wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa reli kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA) katika miaka ya 1970 wakati China ilipotuma wataalamu wake kusaidia ujenzi wa reli hiyo kwa ajili ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika na kukuza maendeleo.

    Makaburi hayo yaliyopo Majohe, Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam yamezikwa wataalamu wa nchini China waliofariki wakati wa ujenzi kwa sababu mbalimbali ikiwemo milipuko, Magonjwa na mengineyo.

    Mapema Asubuhi, viongozi hao wlaianza kwa kutoa heshima zao katika makaburi hayo kisha zikapigwa nyimbo za taifa kwa nchi hizo mbili na baadaye kuzungumza kisha kwa pamoja wahudhuriaji wote waliinama na kutoa heshima kisha kupewa maua waliyoweka kwenye makaburi ya mashujaa hao toka China.

    Balozi Ke anasema wanajeshi wa China, wataalam, watendaji katika kampuni za China zilizopo nchini na watanzania wameungana na serikali ya Tanzania na wadau kutoka sekta mbalimbali kuwakumbuka wataalam na wafanyakazi waliopoteza maisha yao.

    Alisema TAZARA ni alama ya Urafiki wa China na Afrika kwani wakati China ikisaidia ujenzi wake ilikuwa katika wakati mgumu kiuchumi lakini ilijitoa kusaidia nchi za Afrika kupata uhuru kwa kutumia reli hiyo.

    Alisema katika ujenzi wa reli hiyo zaidi ya raia wa China 50,000 walifanya kazi pamoja na wazambia na Tanzania kujenga reli hiyo katika kipindi kisichopungua miaka sita na hatimaye kuipa jina reli hiyo kama Reli ya Uhuru au Reli ya urafiki.

    Anaeleza kuwa katika ujenzi huo, zaidi ya wataalamu na wafanyakazi wa China zaidi ya 50 walipoteza maisha yao kwa magonjwa,milipuko na ajali mbalimbali ikiwemo kushambuliwa na nyuki na kuzikwa katika eneo hilo la Makaburu Majohe,Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam

    Anabainisha kuwa kijana aliyepoteza maisha akiwa na umri mdogo ni Jin Chengwei (22) huku zaidi ya watanzania zaidi ya 100 nao walipoteza masiaha ambao pia wanawakumbuka kwa ushujaa wao.

    Anasema kwa miaka 40, TAZARA imekuwa ikitoa mchango mkubwa wa maendeleo ya uchumi na kijamii kwa Tanzania na Zambia ambapo mpaka sasa China imetuma wataalamu wa awamu 16 wenye wataalam 2800 ya wahandishi na wataalamu.

    Tangu kukamilika 1975, TAZARA ilisafirisha tani milioni 29 za bidhaa na abiria milioni 49 hivyo kuunganisha nchi za Mashariki na kusini mwa Afrika.

    China imeendelea kusaidia Tanzania na Afrika katika Nyanja mbalimbali, nchini na watu wake kwa kampuni za China kujenga miundombinu mbalimbali nchini ikiwemo barabra, madaraja, na usambazaji maji hivyo zaidi ya ajira za moja kwa moja 150,000 zimezalishwa nchini.

    Anabainisha kuwa katika kuwaenzi raia hao wa China wataendelea kuiboresha reli ya Tazara kuendelea kufanya kazi ili kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China.

    Kabuni akitoa salamu zake za Tanzania anasema wachina waliokufa katika ujenzi wa reli hiyo walionesha undugu wa kweli ili kusaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa katika kupigania uhuru.

    "Reli hii ilikataliwa kujengwa na benki ya dunia na wafadhili wengine wa Magharibi lakini Hayati Mwalimu Nyerere aliomba China waliokubali na kuleta wataalamu na kujenga reli iliyosaidikia ukombozi wa nchi za kusini, lakini baadhi yao wakiwemo watanzania, Wazambia na wachina walikufa wakiwa katika ujenzi "anasema.

    Kabudi anabainisha kuwa raia wa China 64 walizikwa eneo hilo na wengine Mpika Zambia ambapo wanakumbukwa kwa upendo na ushujaa wao.

    Alisema Serikali inaangalia namana ya kuwaenzi watanzania na wazambia zaidi ya 100 walizikwa katika maeneo ya kwao kutokana na kufariki na kupelekwa katika jamii zao ili kujenga mnara wa kuwakumbuka kama wlaivyo mashujaa wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako