• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Klabu bingwa Afrika-Simba, Mazembe shoo ya kibabe, Mamelodi yatoa dozi nzito kwa Al Ahly

  (GMT+08:00) 2019-04-08 08:54:57

  Timu ya Simba ya Tanzania imetoka suluhu ya bila kufungana na TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika iliyopigwa jumamosi uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na watarudiana mjini Lubumbashi April 13 nchini DRC.

  Timu zote zilicheza kwa kuviziana kutafuta mabao huku zikicehza mchezo mzuri lakini zilishindwa kutengeneza nafasi za kufunga. Nahodha wa Simba John Bocco alikosa penalti dakika ya 14 ya mchezo. Samba wataondoka wikiendi inayokuja kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Lubumbashi DRC.

  Matokeo ya mechi zingine, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeimwagia mvua ya magoli Al Ahly ya Misri kwa goli 5-0, nayo Horoya AC imetoshana nguvu ya bila kufungana na Wydad Casablanca, huku Esperence imeifunga CS Constantine kwa bao 3-2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako