• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uvumbuzi wa sayansi na teknolojia zaelekeza maendeleo yenye sifa bora ya Beijing

  (GMT+08:00) 2019-04-08 17:25:37

  Uchumi wa China umebadilika na kupata maendeleo yenye sifa bora kutoka katika kipindi cha ongezeko la kasi katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa maendeleo yenye sifa bora yamekuwa na umaalumu muhimu kwa maendeleo ya Beijing, na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia umekuwa msingi muhimu.

  Kampuni ya Sayansi na Teknolojia ya Kuang Shi iliyoko eneo la Zhongguancun, mjini Beijing, ambayo ilianzishwa mwaka 2011 ni kampuni ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu. Ilichaguliwa kuwa moja kati ya kampuni kubwa kumi duniani ya akili bandia. Kiini cha teknolojia za kampuni hiyo ni uwezo wa akili bandia unaohusisha utambuzi wa sura, mwili wa binadamu, ishara ya mikono, kitambulisho, pamoja na picha.

  Kampuni hiyo inaona kuwa uwezo wa akili bandia hautachukua nafasi ya binadamu, bali ni njia ya kufanya uboreshaji, ambao utarahisisha kazi na maisha ya watu na kuongeza ufanisi ili kutoa mchango mkubwa kwa jamii ya binadamu. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Xie Yinan anasema:

  "Hivi sasa tunaweza kubadilisha vitu vinavyoonekana kuwa takwimu zinazoweza kutumika kwenye viwanda vinavyohusika, ili kuongeza ufanisi mkubwa zaidi. Ndiyo maana naona kuwa uvumbuzi ni hatua ya kuongeza ubora na kupunguza gharama za uzalishaji."

  Kwenye eneo la Zhongguancun mjini Beijing, kuna kampuni nyingine nyingi kama kampuni hiyo ya Kuang Shi. Mwaka 2018 idadi ya kampuni za sayansi na teknolojia ya kisasa kwenye eneo hilo ilizidi elfu 22, pato la jumla limezidi yuan trilioni 5.8, sawa na dola za kimarekani bilioni 866, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11. Idadi ya maombi ya hataza ilifikia elfu 86, ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.

  Kampuni ya data ya Jiu Ci Fang inayoshughulikia uendeshaji wa raslimali za data ina matumaini ya kuhimiza data kuwa mali yenye thamani kubwa zaidi. Naibu meneja mkuu wa Kampuni hiyo Bibi Lang Peipei anasema:

  "Mapato ya kampuni yetu kwa mwaka jana yalizidi dola za kimarekani milioni 104. Kati ya wafanyakazi zaidi ya elfu 2 wengi wanashughulikia utafiti na uendelezaji, tulipata hataza zaidi ya 200, na kuandaa majukwaa 500 ya data ya jumla kwa kushirikiana na serikali za ngazi mbalimbali kote nchini."

  Kampuni hiyo inaona kuwa matumizi mazuri ya takwimu hizo yatasaidia kuboresha shughuli za kijamii, mabadiliko ya muundo wa ongezeko la uchumi na kuchangia maendeleo yenye sifa bora ya uchumi nchini China.

  Mji wa Beijing umeyachukulia maendeleo ya uvumbuzi kuwa njia muhimu ya kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya uchumi, kujenga majukwaa ya utafiti na uendelezaji kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu, kutoa huduma zinazohusika ili kutimiza uoanishaji wa vipande vyote kwenye mnyororo wa uvumbuzi wa teknolojia, na kuhimiza njia ya maendeleo yenye sifa bora ya uchumi wa Beijing iwe pana na wazi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako