• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa na Ujerumani zapendekeza umoja wa pande nyingi na China kuunga jitihada za kila upande

    (GMT+08:00) 2019-04-08 19:49:48

    Waziri mkuu wa Ufaransa na chansela wa Ujerumani wakihudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamependekeza kwa pamoja kuanzisha umoja wa pande nyingi na kupanga kuanzisha umoja huo rasmi wakati wa mkutano mkuu wa 74 wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Septemba. Na msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Lu Kang amesema China inaunga mkono jitihada za jumuiya ya kimataifa zikiwemo Ufaransa na Ujerumani katika kulinda utaratibu wa pande nyingi.

    Bw. Lu ameongeza kuwa wakati wa ziara ya Rais Xi Jinping wa China nchini Ufaransa, alihudhuria sherehe ya kufungwa ya baraza la usimamizi wa dunia wa China na Ufaransa kwa pamoja na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel na mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker, na kueleza mtazamo wa China kuhusu kulinda utaratibu wa pande nyingi, kuimarisha mazungumzo na ushirikiano ya kimataifa, kutatua kwa pamoja masuala ya ukosefu wa utawala, uaminifu, amani, na maendeleo, na kuboresha usimamizi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako