• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajiunga na kigezo cha ujumla cha Barclays cha Bloomberg

    (GMT+08:00) 2019-04-08 20:10:48

    Dhamana za ndani na dhamana za benki zisizo za kibiashara za China zinazotumia sarafu ya RMB hivi karibuni zimeorodheshwa kwenye kigezo cha ujumla cha Barclays cha Bloomberg. Mjumbe wa kwanza wa shirika la fedha la kimataifa IMF Bw. Alfred Schipke, amesema hii ni hatua muhimu kwa China kujiunga na mfumo wa fedha wa kimataifa. Vyombo vya habari vinavyojulikana duniani kama CNBC vimesisitiza kuwa hii ni ishara ya China kufungua zaidi soko lake la fedha. … ana maelezo zaidi.

    Kigezo cha ujumla cha Barclays cha Bloomberg ni moja ya mashirika matatu makubwa zaidi ya kutoa vigezo vya dhamana duniani. Habari zinasema, hivi sasa mali za kimataifa zenye thamani ya dola trilioni 5 za kimarekani zinafuatilia kigezo hicho. Kuorodheshwa kwa dhamana za China kwenye kigezo hicho kunamaanisha kuwa wawekezaji wanaofuatilia kigezo hicho wanaweza kuwekeza dhamana hizo na kuleta mitaji mingi zaidi katika soko la China. Uchambuzi umesema, kujiunga na kigezo hicho kwa dhamana za China, kutokana na mitaji ya kimataifa kuna imani na soko la fedha la China.

    Kwanza, sarafu ya China RMB inaendelea kuwa sarafu ya kimataifa. Mwezi wa Oktoba mwaka 2016, RMB iliwekwa kwenye kundi la sarafu ya SDR ya shirika la IMF. Baada ya hapo, hadhi ya sarafu ya akiba ya China ilizidi kutambuliwa na nchi mbalimbali duniani, akiba ya sarafu ya China iliyoko kwenye benki kuu za nchi za kigeni imeongezeka kwa asilimia 100. Wakati huohuo, mahitaji ya RMB kwa wawekezaji wa kigeni pia yanaongezeka.

    Pili, nguvu ya ushindani ya dhamana za China inaongezeka katika pande za thamani na kiwango cha faida. Mwishoni mwa Februari mwaka huu, thamani ya dhamana zilizosalia kwenye soko la China ilifikia dola trilioni 13 za kimarekani, ambalo limekuwa soko kubwa la tatu za dhamana duniani likizifuata Marekani na Japan. Kwa upande wa kiwango cha faida, kiwango hicho cha dhamana za ndani za China zenye ukomo wa miaka 10 kiko juu kuliko za Marekani, Ujerumani na Japan. Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Bloomberg nchini China Bw. Li Bing, hivi karibuni alidokeza kuwa mwaka jana kiwango cha faida kwenye vigezo vya Barclays vya Bloomberg kuhusu China kilifikia asilimia 3.45 huku kiwango hicho cha Marekani kikifikia asilimia 0.01. Takwimu ni mwongozo mzuri zaidi wa uwekezaji.

    Kama rais Xi Jinping wa China alivyosema mwanzoni mwa mwaka huu kwamba, China yenye mzunguko wa fedha itakuwa na uhai mkubwa zaidi wa kupata ustawi na maendeleo. Kufungua zaidi kwa soko la dhamana la China, hakika kutachangia katika kuhimiza uanuai wa mali za kimataifa na kuhakikisha uchumi wa dunia nzima unapata maendeleo mazuri na kwa utaratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako