Rais Xi Jinping wa China leo ameshiriki kwenye shughuli ya kupanda miti mjini Beijing, akisisitiza kuwa inapaswa kuenzi maadili ya jadi ya China katika kupenda, kupanda na kutunza miti, na kuhimiza harakati za kupanda miti nchini kote ili kupata mafanikio yenye ufanisi.
Rais Xi amesema mwaka huu inatimia miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Siku ya kupanda miti nchini China. Katika miaka hiyo 40, eneo la misitu hapa China limeongezeka mara moja hivi, na China imetoa mchango mkubwa zaidi katika ongezeko la idadi ya miti duniani. Hata hivyo amesema bado China inakabiliwa na changamoto za upungufu wa misitu na hali mbaya ya mazingira ya kiuumbe.
Amesisitiza kuwa jamii inatakiwa kuhimiza harakati ya kupanda miti nchini kote na kuboresha mazingira ya makazi ya wananchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |