• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Raga: Serikali ya Kenya yaahidi kuwasaidia Chipu wa Kenya baada ya kuibuka mabingwa wa Afrika U-20

  (GMT+08:00) 2019-04-09 08:22:27

  Serikali ya Kenya imeahidi kusaidia timu ya Chipu ya Kenya kushiriki raga ya dunia ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 ya daraja ya pili baada ya kuichabanga Namibia kwa alama 21-18 katika fainali ya mchezo huo wa bingwa wa Afrika jijini Nairobi.

  Katibu wa wizara ya michezo Kirimi Kaberia amesema serikali ya Kenya itaisaidia timu hiyo maandalizi yake ya Brazil katika michuano hiyo ya dunia.

  Kenya inaungana na wenyeji wa mashindano ya dunia Brazil pamoja na Hong Kong (Asia), Uruguay (Amerika Kusini), Ureno (Ulaya), Tonga (Oceania) na Japan iliyotemwa kutoka mashindano ya dunia ya daraja ya juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako