• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kiprop ashinda mbio za riadha za Vienna kwa mara ya tatu

    (GMT+08:00) 2019-04-09 08:20:52
    Nancy Kiprop ametwaa taji la mbio za riadha za mjini Vienna kwa mwaka wa tatu mfululizo baada ya kushinda makala ya 36 kwa rekodi mpya ya saa 2:22:12 nchini Austria.

    Kasi ya Mkenya huyo ni dakika moja na sekunde 35 bora kuliko rekodi ya awali ya saa 2:23:47 ambayo Muitaliano Maura Viceconte amekuwa akishikilia tangu mwaka 2000.

    Kwa upande wa wanaume, Vincent Kipchumba wa Kenya amerejesha nchini Kenya taji la Vienna, imemchukua saa 2:06:56 kuibuka mshindi mbele ya Mswizi Tadesse Abraham aliyetumia saa 2:07:24 na mganda Solomon Mutai aliyemaliza kwa kutumia saa 2:08:25. Zaidi ya wanariadha 41, 000 kutoka mataifa 110 walishiriki makala hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako