• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi wa Sudan asema jeshi la ulinzi ni kiini cha usalama na ulinzi wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-04-09 08:52:16

    Waziri wa ulinzi wa Sudan Bw. Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf amesema, jeshi la ulinzi la nchi hiyo ni kiini cha amani na ni mlinzi wa usalama, umoja na uongozi wa taifa hilo.

    Bw. Ibn Auf amesema hayo jana alipokutana na viongozi wa jeshi la nchi hiyo mjini Khartoum. Amesema usalama wa nchi hiyo, wananchi wake pamoja na rasilimali zake, ni jukumu la jeshi hilo, na kwamba historia haitawasamehe viongozi wa jeshi kama watashindwa kulinda usalama wa nchi yao.

    Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa wananchi wa Sudan kujizuia, wakati nchi hiyo ikikumbwa na maandamano makubwa. Msemaji wa Katibu Mkuu huyo Bw. Stephane Dujarric amesema, Bw. Guterres anafuatilia kwa makini maandamano yanayoendelea nchini Sudan, na kutaka pande zote zijizuie ili kuepuka vurugu.

    Watu sita wameuawa tangu maandamano yaanze katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako