• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yaanza kuwalipia fidia wazungu waliokuwa wamiliki wa mashamba ya kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-04-09 09:50:49

    Serikali ya Zimbabwe itawalipia malipo ya awali wazungu waliokuwa wamiliki wa mashamba ya kibiashara hivi karibuni, kama fidia ya kuchukuliwa ardhi zao katika mageuzi ya ardhi.

    Tume maalum inayohusisha maofisa wa serikali na wawakilishi wa wazungu hao inafanya tathmini ya mashamba hayo ili kujua kiasi cha fidia itakayolipwa.

    Wakati huohuo, Chama cha Wakulima wa Kibiashara na Tume ya Fidia wanaendelea na mchakato wa kutambua na kuwasajili waliokuwa wamiliki wa mashamba wanaotaka kushiriki kwenye mpango wa muda wa malipo ya awali.

    Habari zinasema, malipo hayo yatatolewa tu kwa wakulima wa zamani wanaokabiliwa na hali mbaya ya kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako