• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa mkutano wa uzinduzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ya China uliofanyika leo hapa Beijing.

    (GMT+08:00) 2019-04-09 12:32:17

    Rais Xi amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita. Amesema China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, na Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, na watu wa pande hizo mbili wana urafiki wenye historia ndefu. Amesema kutokana na hali mpya, kuzidisha urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika si kama tu kutawanufaisha watu wa pande hizo mbili, bali pia kutatoa mchango zaidi kwa ajili ya shughuli za amani na maendeleo duniani.

    Rais Xi amesema kuanzishwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ya China, ni hatua muhimu ya kuongeza mawasiliano ya ustaarabu kati ya China na Afrika, na ametaka taasisi hiyo itoe mchango kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako