• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Ufadhili wa China na benki ya dunia kusaidia Chuo cha Taifa cha Usafirishaji 

    (GMT+08:00) 2019-04-09 17:07:00
    Tanzania imenufaika na ufadhili wa dola milioni 83.5 kutoka Benki ya Dunia na China kwa ajili ya mpango wa kukipandisha hadhi Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa Chuo Kikuu.

    Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imekabidhi eneo la hekta 60 kwa ajili ya mpango huo.

    Akizungumza baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa KIA, Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa, alisema, Benki ya Dunia imetoa Dola za Marekani milioni 21.5 nayo China imetoa ufadhili wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 62.

    Kwa mujibu wa Profesa Mganilwa gharama za kumsomesha rubani nje ya nchi ni zaidi ya Sh. milioni 200, hivyo ujio wa chuo hicho katika Mkoa wa Kilimanjaro utapunguza gharama hizo kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako