Hali hiyo imetokana na bidhaa zisizo za vyakula kama vile mavazi na viatu, kodi ya pango, mafuta ya taa, mkaa, kuni, huduma za afya zimechangia kuongezeka kwa mfumuko huo.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu, imeongezeka kidogo ikilinganishwa na Februari.
Alisema kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia Machi mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |