• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yaendelea kuingilia kati mambo ya Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2019-04-09 19:05:35

    Hivi karibuni, hali ya Mashariki ya Kati inabadilika sana. Leo uchaguzi wa Bunge la Israel umeanza. Kabla ya hapo, rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kutambua Israel kudhibiti mamlaka ya milima ya Golan na kupingwa na jumuiya kimataifa. Lakini uamuzi huo wa rais Trump unaweza kumsaidia waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu kushinda tena kwenye uchaguzi huo. Wakati huohuo, rais Trump amelitangaza jeshi la Iran kuwa ni kundi la kigaidi, na hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kulichukulia jeshi la taifa la nchi moja kuwa ni kundi la kigaidi. Matukio hayo mawili yameonesha kuwa mkakati wa Marekani kwa Mashariki ya Kati umebadilika haraka, na hatua za upande mmoja huenda zitaleta mapigano na kuvuruga amani ya dunia.

    Uamuzi wa rais Trump kutambua mamlaka ya Israel kwa milima ya Golan, umepingwa kithabiti na jumuiya ya kimataifa. Nchi wajumbe wa kudumu na wasio wa kudumu 14 isipokuwa Marekani wote wanapinga uamuzi huo. Chanzo cha Marekani kufanya uamuzi huo ni kwamba mkakati wa Marekani kwa Mashariki ya Kati umebadilika. Tangu rais Trump aingie madarakani, kundi la wanasiasa wenye msimamo mkali limeanza kudhibiti mkakati kwa Mashariki ya Kati. Marekani imechukua kuzidisha nguvu ya Israel na kuitenga Iran na nchi nyingine kama kiini cha mkakati huo, badala ya kuhimiza mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel. Uamuzi huo wa rais Trump unalenga kuzidisha nguvu ya Israel na kuisaidia nchi hiyo kuwa na nguvu kubwa zaidi ya kimkakati na kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Iran imezidi kuwa na ushawishi mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati. Ripoti ya usalama ya Marekani imesema, Iran ina uhusiano wa karibu na Syria, Iraq, kundi la Hezbollah la Lebanon na kundi la Hamas la ukanda wa Gaza, huku ikiunda mzunguko wa kundi la Shia unaoizingira Israel na kuleta tishio kubwa kwa usalama wa Israel na Marekani. Hivyo Marekani inaichukulia Iran kama hatari kubwa na kuanzisha tena vikwazo dhidi ya Iran, baada ya kujitoa kwenye makubaliano ya suala la nyuklia la Iran, ikionesha nia thabiti ya kuizuia nchi hiyo.

    Vita vilivyoanzishwa na Marekani nchini Afghanistan na Iraq sio tu vimeifanya nchi hiyo kudidimia katika hali ngumu za nchi hizo mbili, bali pia vimeleta mazingira mazuri kwa ugaidi na kuzuia mchakato wa amani na maendeleo ya Mashariki ya Kati. Hivi sasa hatua za upande mmoja zilizochukuliwa na Marekani ikipuuza sheria ya kimataifa na kanuni za kimataifa, zimeleta tena vurugu katika eneo la Mashariki ya Kati. Kutokana na juhudi za jumuiya ya kimataifa za kuhimiza mchakato wa amani, hatua hiyo imeenda kinyume na historia na kutishia amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako