• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Uingereza lapitisha mswada wa kuhimiza kurefusha muda wa kujitoa Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-04-09 19:09:32

    Bunge la Uingereza limepitisha rasmi mswada wa kumwagiza waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May afanye mazungumzo tena na Umoja wa Ulaya ili kurefusha muda wa kujitoa Umoja wa Ulaya, la sivyo Uingereza itakabiliwa na kujitoa bila makubaliano tarehe 12. Mswada huo umesainiwa na Malkia Elizabeth II na kuwa sheria rasmi.

    Kwa mujibu wa marekebisho hayo, bunge la Uingereza linaweza kutoa mwito kwa waziri mkuu kuhusu muda utakaorefushwa katika kujitoa Umoja wa Ulaya. Hata hivyo kama Umoja wa Ulaya unaweka tarehe mpya ya Brexit, bunge la Uingereza haliruhusiwi kutoa maoni tofauti na kumfanya waziri mkuu afanye mazungumzo tena na umoja huo.

    Bibi Theresa May aliwasilisha ombi tarehe 5 kwa mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw Donald Tusk, akitaka kuahirisha tarehe ya Brexit hadi tarehe 30 mwezi Juni. Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya watafanya mkutano wa kilele wa dharura tarehe 10 mwezi huu kujadili ombi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako