• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yazindua mpango wa kuongeza idadi ya watalii kutoka China

    (GMT+08:00) 2019-04-09 19:40:34

    Zimbabwe imezindua mpango wa mafunzo ya kujiandaa na China ili kuvutia watalii kutoka China, nchi ambayo mwaka jana ilitumia zaidi ya dola bilioni 100 za kimarekani kutokana na watalii waliosafiri nje.

    Hata hivyo Zimbabwe ilipata sehemu ndogo tu ya watalii wa China, kwa kuwapokea watalii elfu 19 tu. Mpango huo unaifanya Zimbabwe kuwa moja ya nchi 45 kwenye mpango wa kujiandaa kuwapokea watalii wa China.

    Waziri wa mazingira, Utalii na sekta ya huduma Bibi Prisca Mupfumira amesema katika miaka kadhaa iliyopita idadi ya watalii kutoka China imekuwa ikiongezeka. Amesema kwa sasa China ni nchi muhimu kwenye soko la utalii, na yeyote atakayeipuuza China itakuwa hasara kwake. Ametoa mfano kuwa idadi ya watalii kutoka China imeongezeka kutoka 14,407 kwa mwaka 2017, na kufikia 19,428 kwa mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako