• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kutoa tathmini juu ya mazingira ya biashara katika miji 40

  (GMT+08:00) 2019-04-09 19:59:57

  Wakuu wa Wizara ya fedha ya China na Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China leo hapa Beijing wameeleza kuwa, mwaka huu China itatoa tathmini juu ya mazingira ya biashara katika miji 40 kote nchini, na kuhimiza utungaji wa sheria na kanuni zinazohusika, ili kujenga mazingira ya biashara yawe ya kisheria, kimataifa na yenye urahisi zaidi.

  Katika miaka ya hivi karibuni, China imeboresha mazingira ya biashara kwa dhahiri kupitia kukuza mageuzi kwa pande zote, hatua ambayo imehamasisha uhai wa soko na uwezo wa kiuvumbuzi wa jamii. Kwa mujibu wa ripoti kuhusu mazingira ya biashara ya dunia ya mwaka 2018 iliyotolewa na Benki ya Dunia, nafasi ya China imepanda kutoka 78 hadi 45, na China imekuwa moja kati ya makundi ya kiuchumi ambayo mazingira ya biashara yameboreshwa kwa kiasi kikubwa zaidi.

  Naibu waziri wa fedha wa China Bibi Zou Jiayi anasema:

  "Mwaka huu tutachukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kupunguza hatua za ukaguzi na kuthibitisha mipango ya ujenzi inayohusu miradi ya ujenzi isiyo na hatari kubwa mjini Beijing na Shanghai, na kufanya mageuzi kadhaa ya kurahisisha hatua zinazohusu biashara za kimataifa."

  Pia ameongeza kuwa wizara hiyo itafanya marekebisho ya sheria zinazohusika kwa kushirikiana na Kamati ya kutunga sheria ya Bunge la umma la China, ili kujenga mazingira mazuri ya kisheria ya biashara.

  Naibu katibu mkuu wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhou Xiaofei ameeleza kuwa, mwaka jana China ilianzisha utaratibu wa vigezo vya mazingira ya biashara, na kutoa tathmini juu ya miji 22 kote nchini. Mwaka huu maeneo hayo yataongezeka na kufikia miji 40, ili kujenga mazingira ya biashara yawe na ufanisi zaidi, utulivu na uwazi, na ushindani wenye usawa.

  Naibu mkuu wa Idara kuu ya usimamizi wa soko ya China Bibi Gan Lin anasema:

  "Inatakiwa kuondoa kanuni zinazokwamisha maendeleo ya kampuni binafsi kwa mujibu wa mahitaji ya ushindani wenye usawa; kufanya ukaguzi wa makini kuhusu ukiukwaji wa kanuni ya ushindani wenye usawa na kufanya mageuzi kukamilisha utaratibu wa ukaguzi na kujifunza uzoefu wa kisasa wa kimataifa katika sekta hiyo ili kuhakikisha ushindani wenye usawa kwa hatua zenye ufanisi zaidi, na kuboresha mazingira ya biashara."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako