• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China awasili Croatia kwa ziara rasmi

    (GMT+08:00) 2019-04-10 09:00:18

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amewasili Croatia jana kwa ziara rasmi, na pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa nane wa viongozi wa China na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati (CEECs) utakaofanyika katika mji wa pwani Dubrovnik.

    Bw. Li Keqiang ni waziri mkuu wa kwanza wa China kufanya ziara nchini Croatia tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 27 iliyopita. Bw. Li Keqiang amesema anatarajia kuwa ziara yake itaimarisha urafiki kati ya China na Croatia, kuinua kiwango cha kuaminiana kisiasa, kuunganisha zaidi sera na mikakati yao ya maendeleo, na kupanua ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili, ili kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Croatia ufikie ngazi mpya.

    Bw. Li amesema ushirikiano kati ya China na nchi 16 za CEEC umeonesha mwelekeo mzuri, huku maendeleo makubwa yakipatikana kwenye nyanja mbalimbali, ikiwemo uchumi na biashara, uwekezaji, fedha, miundombinu, kilimo na mawasiliano ya kiutamaduni kati ya watu wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako