• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gantz atangaza ushindi katika uchaguzi wa wabunge wa Israel

    (GMT+08:00) 2019-04-10 09:07:17

    Benny Gantz, mpinzani mkuu wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza ushindi katika uchaguzi wa wabunge na kuapa kuhimiza umoja nchini humo. Kwenye makao makuu ya chama chake kilichoundwa upya cha Blue and White mjini Tel Aviv, Gantz amesema atakuwa waziri mkuu wa kila mtu, wala sio wa wale waliompigia kura tu, na anafikiria jinsi ya kushirikiana na watu wa vyama vingine, na kumshirikisha kila mtu kwenye majadiliano. Maoni ya wapiga kura yaliyotangazwa kwenye televisheni tatu kuu za Israel yanaripoti matokeo yanayokinzana. Naye Bw. Netanyahu pia ametangaza ushindi katika uchaguzi huo ambao matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako